Pages

Friday, 28 March 2025

Kilimo Bora cha Migomba

1. Maeneo Yanayofaa
Migomba hustawi vizuri kwenye maeneo yenye joto la 15°C - 35°C, mvua ya kutosha (1,200 - 2,500 mm kwa mwaka) na udongo wenye rutuba, wenye pH ya 5.5 - 7.0.

2. Aina za Migomba
Musa acuminata – Migomba ya ndizi tamu kama Cavendish 
Musa balbisiana – Migomba ya ndizi za kupika kama Mzuzu
Hybrid varieties – Kama FHIA-17 na FHIA-25, zinazostahimili magonjwa

3. Upandaji
.. Chagua miche bora isiyo na magonjwa
.. Panda kwa nafasi ya 3m × 3m ili kuepuka ushindani
.. Hakikisha shimo lina urefu wa 60cm na upana wa 60cm

4. Mbolea
Samadi au mboji (debe 2 kwa shimo)
Mbolea za viwandani: NPK (10:10:20) kwa ukuaji na mavuno bora
Urea kuongeza nitrojeni kwa majani yenye afya

5. Magonjwa na Wadudu
Mnyauko wa bakteria (BXW) – Dhibiti kwa kukata migomba iliyoathirika
Panama disease (Fusarium wilt) – Panda aina sugu za ndizi
Nematodes – Tumia mbegu safi na udhibiti kwa majani yaliyooza

6. Mavuno
Ndizi huanza kuzaa baada ya miezi 9 - 12, na mavuno yanaweza kuendelea kwa miaka 5 - 7.

Kwa mafunzo zaidi ya kitaalamu, vitabu na darasa vinaendelea! Tuma inbox au Comment kwa maelezo zaidi.

No comments:

Post a Comment